Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa.
Na Gladness Mallya, GPL
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa
warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini
ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika
suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu
sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba.