MKUU
wa wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, Mery Tesha ameagiza
uchunguzi ufanyike na kisha waliousika kuzuia
mafunzo ya mgambo yasifanyike kisiwani Ukara wakamatwe na
kufikishwa mahakani.
Akifunga
mafunzo ya mgambo katika kata ya Mriti jana
alisema mafunzo hayo yalipangwa kufanyika
kisiwani Ukara lakini baadhi ya viongozi wa ngazi
za vijiji na kata kisiwani hapo walizua.
Akifafanua
alisema baadhi ya viongozi wa kisiasa wa ngazi hizo
waliwashawishi vijana waliojiandikisha kushiliki
mafunzo hayo wakatae vingine walipwe posho na
kupewa chakula cha kuacha nyumbani kwao.
Kufuatia
hali hiyo mafunzo hayo ya miezi minne yaliyopangwa
kuanza Julai mwaka huu hayakunyika na
kuulazimu uongozi kuamisha mafunzo hayo katika kata ya
Mriti ambapo pia ilitumika sheria kuwapata
washiliki wa mafunzo hayo.
Kufuatia
hali hiyo Tesha amesema hatavumilia mtu yeyote
atakayethibika kuzuia shughuli halali za serikali na kuongeza
kuwa tayari ameagiza viongozi na hata mtu yeyote
aliyeusika kuzuia mafunzo ya mgambo yasifanyike
kisiwani Ukara akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Awali
katika risala yao iliyosomwa Athuman Bakari
walisema jumla ya vijana 198 wa kata hiyo
waliandikishwa kushiliki mafunzo hayo lakini waliojitokeza na
kushiliki mafunzo hayo ni 17 pekee.
Walisema
mbali ya baadhi yao kukosa sifa kwa sababu mbali mbali
zikiwemo ushiliki wa vitendo viovu, magonjwa sugu lakini wengi
wao walitoroka kwa hofu ya kuteshwa na hata kupoteza
muda mwingi wa kufanya shughuri zao za kuwaingizia
kipato.
Wamesema
katika mafunzo hayo wamefanikiwa kupata mafunzo ya ukakamavu,
mbinu za kivita , matumizi ya siraha za moto, Mabomo na usarama wa raia
hata hivyo waliomba kupewa kipau mbele pindi zinapotolewa ajira
katika majeshi ya ulinzi.
