Na Gabriel Kilamlya Njombe
Wafanyabiashara wa Biadhaa Mbalimbali Mkoani Njombe Wametishia Kugomea Utaratibu wa Matumizi ya Mashine Mpya za Risiti za EFD Endapo Serikali Haitowapunguzia Kodi ya Asilimia 18% Pamoja na Kuangalia Uwezekano wa Kupunguza Gaharama za Ununuzi wa Mashine Hizo.
Kauli hiyo Wameitoa Leo Kwenye Kikao cha Wafanyabiashara Hao Kilichoitishwa na Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Tanzania Chamber of Commerce TCCIA Kilicholenga Kujadili namna ya Kukutana na Serikali Kupitia Mamlaka ya Mapato TRA Katika Kupata Ufafanuzi Juu ya Mashine Hizo.
Baadhi ya Wafanyabiashara Hao Ambao Tayari
Wanaendelea Kuzitumia Mashine Hizo Wamesema Kuwa Matumizi ya Mashine Hizo Yamekuwa Yakiwaletea Shida Kubwa Kutokana na Usumbufu Wake Kwani Zimekuwa Zikiharibika Mara kwa Mara na Hata Mafundi wa Kuzitengeneza Hawapatikani.
Akifungua Kikao Hicho Kilichofanyika Katika Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe TCCIA Bwana Oraph Mhema Amewataka Wafanyabiashara hao Kuimarisha Umoja wao Ili Kurahisisha Uwasilishaji Hoja Zao Serikalini Kwa Nia ya Kukuza Uchumi wa Taifa na Wafanyabiashara Wenyewe Tofauti na Ilivyo sasa.
Kwa Upande Wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Bwana Menardy Mlyuka Amesema Kwa Kuwa Serikali Mkoani Njombe Imepanga Kukutana nao Novemba 27 Mwaka Huu Kuzungumzia Suala Hilo Ni Lazima Kama Wafanyabiashara Wakajitokeza Kwa Wingi Ili Kufahamu Dhima ya Serikali Kwa Wafanyabiashara Katika Kilio chao Juu ya Mashine Hizo.
Hivi Karibuni Wafanyabiashara wa Mikoa ya Dodoma,Mbeya na Dar es Salaam Waligomea Kununua Mashine Hizo Kutokana na Gharama Kubwa Ya Shilingi Laki Nane Pamoja na Makato Mbalimbali Yanayotokana na Biashara zao Hali Inayopelekea Kufilisika Mtaji Ilihali Wanakopa Benki na Kwenye Taasisi Nyingine.
