Kufuatia tatizo la kugongwa na kuanguka kwa nguzo za msongo mkubwa
zaidi ya tano katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Afisa Uhusiano wa
Tanesco, Badra Masoud amefunguka na kusema kuwa mafundi wapo kazini
ambapo umeme utarejea kuanzia saa 1:00 usiku.
Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita, Badra alisema hadi
muda huu polisi hawajanikiwa kuwakamata wahusika waliogonga nguzo moja
na kusababisha nyingine kuanguka usiku wa kuamkia leo.
"Tatizo ni kubwa lakini mafundi wetu wapo kazini. tunatarajia hadi
ifikapo saa moja usiku umeme utawaka maeneo yote yaliyoathirika hasa
Kijitonyama," alisema Badra akiliomba jeshi la polisi kuwakamata haraka
wahusika wa tatizo hilo.
Usiku wa kuamkia leo dereva asiyejulikana aligonga nguzo moja ya
umeme jirani na Chuo Cha Posta Kijitonyama iliyoangusha nguzo zingine
tano na kusababisha mlipuko mkubwa wa moto katika Barabara ya Ali Hassa
Mwinyi maeneo ya Bamaga.
CREDITS:GPL