SERIKALI YAPENDEKEZA MAGAZETI YANAYOANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI YAONGEZEWE ADHABU

Serikali imependekeza ongezeko la adhabu kwa magazeti yanayochapisha habari zinazoweza kusababisha uchochezi au uvunjifu wa amani katika jamii kutoka faini ya shilingi elfu 10 na 5 hadi kiasi kisichopungua shilingi milioni 5.
 
Akiwasilisha mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2013, mwanasheria mkuu wa serikali jaji mstaafu Fredrick Werema, amesema marekebisho hayo yanalenga kutekeleza azimio la bunge lililotolewa katika mkutano wa 11 kikao cha 21 ambalo bunge liliazimia serikali kupitia sheria zilizopo ili kuona kama zinatosheleza kuzuia lugha ama kauli za uchochezi.

Wakiwasilisha maoni ya kamati ya katiba, sheria na utawala, pamoja na maoni ya kambi ya upinzani, msemaji wa kamati hiyo Mhe Fakharia Shomar amesema kamati yake inaunga mkono pendekezo la serikali kwa kuzingatia misingi ya vyombo vya habari ni kuelimisha na kuhabarisha si kuleta uchochezi,wakati kambi rasmi ya upinzani bungeni imeitaka serikali kufuta sheria na kutunga sheria mpya itakayojali uhuru wa vyombo vya habari.

Wakichangia mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali baadhi ya wabunge wameitaka serikali kuharakisha kuleta mswada wa sheria vyombo vya habari,huku wengine wakipinga adhabu ya shilingi milioni 5 kwa madai kuwa ni kiwango kikubwa na kutaka serikali kuweka uwiano kwa baadhi ya watu wanaopinga kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.
 
Via ITV Habari 20:00hrs


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo