NEWS ALERT: MBUNGE WA UKEREWE KWA TIKETI YA CHADEMA AFUTIWA DHAMANA NA MAHAKAMA


Mbunge wa Ukerewe kwa tiketi ya CHADEMA, Salvatory Machemli, leo mchana amefutiwa dhamana na Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe na kuamriwa aende ndani hadi tarehe ya kesi yake itakapotajwa tena!

Kesi inayokabili ni ya uchochezi ya mwaka 2010 wakati wa Kampeni, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.


Kesi hii ilifunguliwa mwaka 2012, tayari KUB amemwandikia rasmi katibu wa Bunge na kumjulisha juu ya jambo hilo. Aidha, wananchi wameendelea kutafuta dhamana kwani sharti lililowekwa ni kuwa na hati tatu za nyumba na wadhamini watatu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo