Msafara wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete mkoani Geita, jana umeingia dosari baada ya gari moja lilokuwa kwenye msafara huo kupinduka na kujeruhi watu watano.
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
|
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Geita Lenard Paul ajali hiyo
imetokea leo saa 3 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Nyankumbu
kilomita 3 kutoka makao makuu ya mkoa wa geita.
Kamanda
Paulo amesema gari hilo namba DFP.9730 aina ya Toyota Landcruzer
lililokuwa likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa
(MSD), lilipinduka baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani
hii leo.
Amewataja Waliojeruhiwa
katika ajali hiyo kuwa ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na
Radio Free Afrika, Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda
Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa MSD kanda ya Ziwa
Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.
Kamanda
Paulo amesema majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali ya wilaya ya
Geita kwa ajili ya matibabu na kisha kuruhusiwa huku Mwandishi Peter
Makunga akiwa bado amelazwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea
vizuri.
![]() |
| Askari akilikagua gari. |
| Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita. |
| Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari. source:faraji mfinanga. |
