MR. BLUE AZUNGUMZA NA REDIO CITIZEN YA KENYA KUHUSU UTAPELI UNAOFANYWA KWA JINA LAKE NCHINI HUMO

1395823_10201702445835581_1932598565_nHitmaker wa Mapozi, Mr Blue leo amezungumza na mtangazaji wa Radio Citizen, Willy M Tuva kwenye kipindi cha Mambo Mseto kuhusiana na jinsi ambavyo jina lake limeendelea kutumika kufanya utapeli nchini Kenya.

Gazeti la The Star la Kenya liliandika kuwa staa huyo alitapeli advance ya show mbili za Kenya na kumfanya promota wa show hizo afungue kesi mjini Mombasa na kumuita Mr Blue ni tapeli na kwamba anatafutwa na polisi.


Mr Blue amesema promota huyo aliwasiliana na Mr Blue fake na wakakubaliana kuhusu show hizo lakini baadaye akawa ameingia mitini.


"Mwisho wa siku kumbe sio mimi. Jamaa amekuja kunipigia simu ananilalamikia nikamwambia 'mimi sijui chochote, kwanza sipo kwenye Facebook'", amesema Kabayser. Amesema hakuwa na kitu cha kumsaidia promota huyo kwakuwa alikuwa tayari na show zingine hapa nchini na hivyo asingeweza kuokoa jahazi.

Sikiliza sauti yake hapa akizungumza na redio citizen ya Kenya(credits:bongo 5)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo