MKUU WA WILAYA YA MAKETE AAGIZA ELIMU YA MGAMBO ITOLEWE KABLA YA MAFUNZO KUANZA

 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya Mgambo kata ya Kitulo
 Mgambo waliohitimu wakiwajibika katika gwaride
=====
Kufuatia kukosekana kwa elimu ya umuhimu wa mafunzo ya mgambo kwa jamii, Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro amemuagiza mshauri wa mgambo wilaya ya Makete kuhakikisha wanatoa elimu kwa eneo husika kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo kabla ya kuanza kuyatoa

Mkuu wa wilaya ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kufunga mafunzo ya mgambo kwa kata ya Kitulo wilayani Makete yaliyodumu kwa kipindi cha miezi minne

Mh Matiro amesema anaunga mkono risala ya wahitimu wa mafunzo hayo kuwa kumekuwa na ushiriki mdogo wa wananchi kushiriki mafunzo hayo kwa kuwa hawaoni umuhimu huku wengine wakishiriki kuwahimiza wananchi kuyasusia mafunzo hayo kwa madai kuwa hayana faida

"Sasa naaginza kwako mshauri wa mgambo wilaya, kuanzia leo hakuna kutoa mafunzo ya mgambo kwenye eneo bila kutoa elimu kwa wananchi wake ili wafahamu umuhimu huo na sheria ya nchi inasemaje kuhusu mgambo" amesema Mkuu wa wilaya

Mh. Matiro amesema kuanzia sasa anaimani vitendo vya kihalifu vinavyoshika kasi katika kata ya Kitulo vitakwisha kwa kuwa ulinzi umeongezeka na wananchi wataishi kwa amnai endapo wanamgambo hao watatimiza wajibu wao wa kuwalinda wananchi na mali zao

Wakisoma risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Festo Ngogo, wanamgambo hao wamesema katika mafunzo hayo wamehitimu 54 ambapo wengi walitoroka mafunzo hayo kutokana na wananchi kuwashawishi na kuwaambia kuwa hayana maana yeyote

Wamesema kwa hivi sasa wanauhakika wataisaidia kata yao kupambana na vitendo vya kihalifu ambayo vinashika kasi katika kata hiyo kutokana na kupita mika mingi bila mafunzo hayo kufanywa kwao

naye mshauri wa mgambo wilaya ya Makete Anthony Mfuse amesema wanamgambo hao wamejifunza mbinu za kivita, ujanja wa porini, huduma ya kwanza na namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali kwani wakati wa mafunzo walishiriku kuzima moto kichaa ulioibuka katika misitu iliyomo kwenye kata hiyo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo