HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA
MKUTANO WA 13 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 09
NOVEMBA, 2013
I: UTANGULIZI
a) Masuala ya Jumla
Mheshimiwa Spika,
1. Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.
1. Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.
Mheshimiwa Spika,
2. Mkutano huu ulijumuisha kazi kubwa zifuatazo:
2. Mkutano huu ulijumuisha kazi kubwa zifuatazo:
Kwanza: Kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2014/2015;
Pili: Kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali
wa Mwaka 2013, [The Written Laws (Miscellaneous Amendments (No. 3) Bill
2013];
Tatu: Kujadili Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao
ya Wastaafu wa Mwaka 2013 [The GEPF Retirement Benefit Bill, 2013]; na
Nne: Kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (The Constitutional Review Act) sura ya 83.
3. Nitumie nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa
kushiriki katika Kamati ya Mipango hapa Bungeni kwa kujadili kwa kina
mapendekezo yaliyowasilishwa na Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa mwaka 2014/2015. Napenda kuwahakikishia kuwa, maoni na ushauri
kama yalivyotolewa na Waheshimiwa Wabunge yatazingatiwa na Serikali
kila moja kwa uzito wake wakati wa maandalizi ya Bajeti ya 2014/2015.
Vilevile niwashukuru kwa kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya
Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu.
b) Maswali
Mheshimiwa Spika,
4. Pamoja na kukamilisha kazi hizo muhimu, pia katika Mkutano huu, jumla ya maswali 120 ya msingi na 305 ya nyongeza ya Waheshimiwa Wabunge yalijibiwa na Serikali. Aidha, Maswali 6 ya msingi na 6 ya nyongeza yalijibiwa kwa utaratibu wa Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.