POLISI WAKINUKISHA JIJINI MWANZA

Wakazi wa jiji la mwanza wapagawishwa na uvamizi FEKI wa Ali-Shabaab uliofanyika ndani ya Hotel ya Gold Crest
 

Wakazi wa jiji la Mwanza juzi  majira ya saa 4 asubuhi waliwekwa njia 
panda na kujawa hofu kubwa kufuatia vikosi vya askari kanzu, FFU, askari
polisi na zimamoto wakiwa na vifaa sambamba na magari yao walipolivamia
jengo la Hotel Gold Crest na kuanza saka saka za kujiweka sawa huku 
wakiendeleza mapambano na jamaa ambao walijipanga mithili ya wahalifu.Hali hiyo ilisababisha magari pikipiki kusimama kwa muda huku 

wananchi wakiingiwa hofu na woga, wengine wakikimbia na baadhi ya 
wafanyabiashara walifunga maduka yao wakifananisha na lile la Westgate la jijini Nairobi nchini Kenya..

Hata hivyo mpaka zoezi hilo linamalizika hakuna mwananchi aliyeweza kubaini kuwa tukio hilo lilikuwa ni la uigizaji, kila mmoja alikuwa 
akisimulia kivyake sekeseke zima, lakini mapango mzima ulikuwa ni 
kuvinoa vikosi vya polisi na Zimamoto juu ya kukabiliana na uhalifu 
kwenye majengo makubwa ya huduma mbalimbali.  







Wateja wa kituo cha mafuta kilichopo karibu na hotel Gold Crest jengo
ambalo ndiko zoezi lilikuwa likifanyika pamoja na wateja wa ofisi za 
PPF, duka la Vodacom Mwanza na Benki ya NMB zilizopo katika jengo hilo 
walikosa huduma kwa muda huku wengine wakitimka maeneo hayo kwa 
tahadhari wakidhani ni live.
Watu wakihaha nao polisi wakiweka ulinzi mkali eneo la tukio.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo