IDD AZZAN AIBUKA KIDEDEA TUHUMA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, GAZETI LA RAIA MWEMA KUMLIPA FIDIA

 
Gazeti la raia mwema limeagizwa kumuomba radhi mbunge wa Kinondoni jijini DSM Iddi Azan kwa kuandika habari za uongo dhidi yake kuwa anajishughulisha na biashara ya dawa za kulevya

Pamoja na hayo pia gazeti hilo limetakiwa kumuita Iddi Azana na kufanya naye mahojiano ya kina kwa namna alivyohusishwa na suala hilo, pamoja na kumlipa gharama zote za mwenendo wa shauri hilo hadi maamuzi hayo yakatoka

Maamuzi hayo yametolewa na baraza la habari Tanzania MCT, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mbunge huyo kuwa hakutendewa haki na gazeti hilo

Mbunge Azan amesema kwa yeye anashukuru sana kwa kuwa licha ya suala hilo kumuathiri, lakini wananchi wake walizidi kumpa ushirikiano kama kawaida huku wengine wakimuombea dua


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo