Moto ukiendelea kuwaka katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Grace Lodge iliyoko katika maeneo ya Kitanzani katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.2. Moto ukiwaka kwa ndani ya nyumba ya kulala wageni ya grace lodge.3.
Wananchi wakishangaa moto ukiendelea kuwaka katika nyumba ya kulala
wageni ya Grace Lodge uliotokea juzi maeneo ya Kitanzani katika
halmashauri ya manispaa ya Iringa.(Picha zote na Denis Mlowe)
======== ========== ==========
NYUMBA KULALA WAGENI YAUNGUA MOTO
Na Denis Mlowe,Iringa
MOTO
mkubwa ambao chanzo chake hakijajulikana uliibuka juzi na kuteketeza
nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Grace Lodge na
kusababisha hasara ya shilingi milioni 225.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi amethibitiisha
kutokea kwa moto huo na uliosababisha hasara kubwa kwa mmiliki wake
Jerida Jackson, Mungi alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana na
hakuna madhara kwa binadamu zaidi ya mali iliyoko katika nyumba hiyo.
Mungi
alisema jeshi la polisi liko katika uchunguzi kwa kushirikiana na
shirika la umeme Tanzania (Tanesco) kuweza kubaini chanzo cha moto huo
na madhara mengine yaliyojitokeza baada ya kuteketea kabisa.
Nyumba
hiyo iliyoko maeneo ya Kitanzani katika halmashauri ya manispaa ya
Iringa inamilikiwa na Jerida Jackson (32) ambaye alizungumza na Tanzania
Daima kuwa thamani ya vitu vilivyoteketea ndani ya nyumnba hiyo ni
zaidi ya Sh 225 milioni huku akifafanua kuwa alipata taarifa za kuungua
nyumba yake kutoka kwa mmoja wa wahudumu waliokuwa wakifanya kazi
katika nyumba hiyo.
Huku
akibubujiwa na machozi alisema (Sijui kitu mimi kuhusu chanzo cha moto
huo sina cha kusema,lakini kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme
tangu Jumatat na hata jana (juzi) kulikuwa na tukio hilo lakini sijui
kama hicho ndicho chanzo ama la”alisema Jackson.
Katika
hatua nyingine wakazi mkoani hapa wamelitupia lawama jeshi la Zima moto
Mkoa wa Iringa wakidai limechelewa kufika eneo la tukio kuuzima moto na
ndio sababu ya nyumba hiyo kuteketea.
Mmoja
wa wananchi hao Hadija Ramadhani alisema tukio la kuchelewa kwa gari
hilo ndiko kumechangia mto kuunguza sehemu kubwa ya nyumba hiyo. Naye Joseph Chengula alisema kikosi cha zima moto kilitumia gari dogo ambalo halikuwa na uwezo wa kuzima moto.
“Mara
ya kwanza wamekuja na gari dogo ambalo halikuwa na uwezo wa kuzima moto
huu,limeishiwa maji na hii sasa ni mara ya tatu linarudia kama
wengetumia hili kubwa lkilifika muda huu ni dhahiri moto usingeangamiza
nyumba kwa kiwango kikubwa hivi. Kwa upande wake Diwani wa kata
ya Kitanzini Jesca Msambatavangu alipengeza ushirikiano ulioonyeshwa na
wananchi wakati wa kuzima moto huo ambao walikuwa wakitumia ndoo kuchota
maji na kubwagia maeneo yaliyoathirika.
Kwa
upande wake Kamanda wa kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kenned Komba
alitetea kitendo cha skari kuchelewa eneo la tukio akidai limetokana na
taarifaza mto kuchelew akufika ofisini kwake.
“Tunayo
namba ya 114,kazi yake ni kupata taarifa za matukio toka popote
yanapotokea lakini kwa leo haikutumika,tumeletewa taarifa na watu
waliokuja na pikipiki tu,lakini pia gari letu kubwa lilikuwa gareji ndio
sababu tumetumia gari ndogo ambayo mafuta maji yaliyopo huisha ndani ya
muda mfupi”alisema Komba.
Komba
alisema hata hivyo kazi waliyoifanya ni kubwa kwani baadaye walipeleka
magari yote eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo.


