BALAA:MAFURIKO YALETA BALAA KAHAMA MKOANI SHINYANGA BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA...!!


Nyumba iliyoingiliwa na maji hadi ndani
Ikiwa ndio mvua za awali za masika zimeanza kunyesha katika mikoa ya Kanda ya ziwa, huenda katika siku zijazo zikaleta madhara makubwa kutokana na tatizo la miundombinu hasa katika wilaya ya kahama.

Hii inafuatia mvua iliyonyesha leo kwa muda wa saa moja tu katika mji wa kahama na kujaza maji katika baadhi ya nyumba za wananchi, nyumba za kulala wageni na hata katika nyumba za maduka ya biashara hasa katika mitaa ya majengo na Nyasubi mjini humo.

Nyumba nyingine ambayo pia maji yamejaa ndani
Katika muda wa takriban saa moja na nusu magari, pikipiki, baiskel na hata watembea kwa miguu walisimama kutokana na kushindwa kuvuka katika maji yaliyojaa katika kalvati na kutapika juu ya barabara.

 Endelea kuangalia matukio katika picha hapa…
Ilikuwa ni balaa tupu
Mfanyabiashara akijaribu kuzibua kalvati liloziba ili maji yatoke katika eneo lake

Maji yanavyotapika juu ya kalvati, tena hapa yamepungua

Maji yalivyojaa barabarani duhhh!!

Kila mmoja natafuta pa kupita

Mitaa hii hakufai

Kupita kwa miguu tatu, Bodaboda tabu

Baadhi ya Familia wakishangaa hali ilivyo

Duhh! Barabara haitamaniki

Sijui gari zitapitaje wakati masika inaendelea
Kiukweli katika hili serikali inatakiwa kuboresha sana Miundfombinu hasa ya Barabara katika mji huu wa madini Kahama!!
 
Chanzo: Faraji Mfinanga via DUNIA KIGANJANI BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo