Balozi
Abraham Isaac Sepetu amefariki dunia mapema leo akiwa katika hospitali
ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi
alioupata hivi karibuni mjini Zanzibar. Balozi Sepetu, ambaye pia ni
baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, hadi anapatwa na
ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. PICHA: Maktaba/GPL
WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, MZEE BALOZI ABRAHAM ISAAC SEPETU
By
Edmo Online
at
Sunday, October 27, 2013