Mwenyekiti wa chama cha waandishi
wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard kulia akitoa msimamo wa
wanahabari dhidi ya gazeti la Rai na mbunge Msigwa leo ,kushoto ni
katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin
Wanahabari Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi wa New habari {2006} Ltd wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai na Bingwa mkoa wa Iringa Mercy Mwalusamba wakati wa kikao cha cha wanahabari mkoa wa Iringa leo kujadili habari zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili
Wanahabari wakifuatilia kwa makini kikao hicho
Wanahabari Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi wa New habari {2006} Ltd wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai na Bingwa mkoa wa Iringa Mercy Mwalusamba wakati wa kikao cha cha wanahabari mkoa wa Iringa leo kujadili habari zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili
Wanahabari wakifuatilia kwa makini kikao hicho
======
WANAHABARI
mkoani Iringa wamekanusha vikali habari zilizoandika na gazeti la
Rai toleo namba 1067 la jumapili wiki iliyopita kuwa wanahabari mjini
Iringa wamehongwa fedha na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa ili
wasiandike habari ya msaidizi wa mbunge Wiliam Lukuvi Bw Thom Malenga
kukamatwa kwa
tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Wahanabari
hao katika kikao chao kilichofanyika leo katika ofisi za klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) mbali ya kukanusha
habari hizo kuwa zimeandikwa kwa lengo la kuchafua tasnia ya habari
mkoa wa Iringa ila bado wanalitaka gazeti la Rai na mbunge wa
jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kuwataja waandishi
waliohongwa na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa
kabla ya wanahabari hao hawajachukua hatua zaidi dhidi ya gazeti
la rai pamoja na mbunge Msigwa.
"Kilichoandikwa
na gazeti la Rai jumapili kuhusu wanahabari Iringa hawajatutendea
haki na wametuvunjia heshima yetu kwa wadau wa habari mkoa wa
Iringa na nje ya mkoa wa Iringa.....ila tunachotaka Rai kuwataja
waandishi hao waliohongwa ili sisi kwa sisi kama wanahabari
kuanza kuchukuliana hatua ....wakishindwa
kufanya hivyo ndani ya siku 14 kuanzia leo jumanne tutawafikisha baraza
la habari Tanzania (MCT)"
Walisema
wanahabari hao katika tamko lao la pamoja lililotolewa na
mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kuwa taarifa hiyo imechafua vibaya
wanahabari Iringa na sio wacache ni wote kutokana na jinsi ambavyo
gazeti hilo lilivyoandika habari hiyo tena mbaya zaidi mwandishi wa
habari hiyo hakuweza kuwatendea haki wanahabari Iringa
hata kwa kuonyesha kuwahoji katika habari yake hiyo.
Leonard
alisema kuwa si kweli kama wanahabari Iringa walishindwa kuandika
habari hiyo ya kukamatwa kwa Malenga isipo kuwa wanahabari Iringa ni
makini na hawakutaka kuandika habari kwa kukurupuka hivyo walitaka
kabla ya kuandika kuweza kumpata msemaji wa kikosi hicho cha kupambana
na ujangili ili kulizungumzia hilo kabla ya kuandika jambo ambalo
wao kama wanahabari walikuwa wakilisikia
mitaani bila kuwa na uhakika.
Uandishi
wa habari mzuri ni pamoja na kuzingatia maadili ya uandishi na sio
kuandika bila ya kuwa na uhakika wa kile unachokiandika .
Hata hivyo alisema
kwa kuwa mbunge Msigwa amenukuliwa katika gazeti hilo kama ndio
msemaji wa jambo hilo wao kama wanahabari watamwandikia barua mbunge
huyo ili kusaidia kuwataja wanahabari waliohongwa pesa vinginevyo
wao kama wanahabari wa mkoa wa Iringa hawatamvumilia mbunge Msigwa
katika hilo .
Pia
alisema kuwa suala hilo kwa sasa ameachiwa mwanasheria wa IPC ili
kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja
na kuwaandikia barua Rai na mbunge Msigwa kuwataka kuthibitisha
ukweli wa kilichoandikwa dhidi ya wanahabari mkoa wa Iringa.