VURUGU ZAIBUKA BAINA YA MEYA WA SERIKALI NA MADIWANI WA CHADEMA ILEMELA

Kikao cha baraza la madiwani la hamshauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza leo kimetawaliwa na vurugu na mabishano hali iliyopelekea kuvunjika kwa kikao hicho.

Vurugu na kurushiana maneno makali, zilianza baada ya meya wa halmashauri ya wilaya hiyo, Henry Matata kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo alipotoa amri ya kuwafukuza kwenye kikao madiwani wawili kutoka chama cha Demokrasi na maendeleo (chadema).


Meya huyo ambaye mefungua kesi mahakamani ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chadema, aliwataka madiwani hao kutoka nje kwa kile alichoeleza kuwa alikwisha wavua wadhifa wa udiwani kwa kitendo chao cha kugomea kuhudhuria vikao vya baraza bila kuiomba ruhusa kwa meya huyo


Vurugu hizo zilipelekea kushindwa kufanyika kwa kikao hicho ambapo madiwani hao wameeleza masikitiko yao kwa serikali kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Meya huyo.

NA JF 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo