Mwimbaji kutoka THT Amini ameelezea pengo liloachwa moyoni
mwake na aliyekuwa mpenzi wake ‘Linah’, pengo ambalo kwa mujibu wake
aliyechukua nafasi hiyo ameshindwa kuliziba.
Mwimbaji huyo ameyatoa yake ya moyoni kupitia Instagram na kuonesha
kuwa bado anamhitaji Linah kwa kuwa ndiye mtu aliyekuwa anampa furaha na
kwamba hakuwahi kumkosea.
Amepost picha inayomuonesha akiwa na Linah, na kuandika,
“Wakati kama huu ukifka uwa namuwaza sana uyu wa pembeni kiukweli ni
mtu ambea aliweza kunipa furaha akuwahi nikosea alifnya ninachokitka ila
nilipo sasa mmmmmh boko miss uuuuu linah kwani nini si nini tu.”