MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA AKITOA SALAAM ZA
SERIKALI KATIKA MKUTANO WA BARAZA KUU LA MADIWANI HALMASHAURI YA MJI
WA NJOMBE
Na Michael Ngilangwa, Njombe
Halmashauri ya Mji wa Njombe Imefanikiwa Kukusanya Mapato ya Ndani Kwa Asilimia 18. 1 Kwa Kipindi cha Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha wa 2013 / 2014 Huku Akitarajia Kuvuka Lengo Ifikapo Juni Mwakani.
Akiongea Wakati wa Kufungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Mwenyekiti Halmashauri Hiyo Edwin Mwanzinga Amewataka Madiwa wa Baraza Hilo Kuongeza Jitihada za Ukusanyaji wa Mapato na Kuziba Myanya ya Ukwepaji Kodi na Ushuru.
Aidha Mwenyekiti Huyo Pia Amewata Madiwani na Wataalam wa Halmashauri Hiyo Kushirikiana Kwa Pamoja Katika Kusimamia na Kutekeleza Miradi ya Maenadeleo.
Akitoa Taarifa Mbalimbali za Miradi Inayotekelezwa na Halmashauri Hiyo
Bwana Mwanzinga Amesema ni Pamoja na Mchakato wa Kupitisha Rasimu ya Mfuko wa Afya ya Jamii na Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mjini Njombe Zoezi Ambalo Limeanza Oktoba 11 Mwaka 2013.
Awali Akitoa Salam za Serikali Kwenye Kikao Hicho Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Amewataka Madiwani Hao Kuongeza Jitihada za Ukusanyaji Mapato ya Ndani na Kusimamia Matumizi Yake, Pamoja na Kuhakikisha Sera na Mipango ya Halmashauri Hiyo Inatekelezwa Kikamilifu.
Halikadhalika Bi. Dumba Amewataka Madiwani Hao Kuhakikisha Wanasimamia Ujenzi wa Kituo cha Kukusanya na Kuhifadhi Matunda Pamoja na Kuwasomesha Wataalam Kwa Ajili ya Kilimo cha Matunda