UHAMISHO WA WACHEZAJI MBALIMBALI BARANI ULAYA

 
- Luis Suarez (26) anawaniwa na Real Madrid kwa dau la £45m.
- Kiungo mshambuliaji
Mesut Ozil (24) huenda akatua Arsenal kwa dau la £42.5m
- Mshambuliaji
Zlatan Ibrahimovic sasa yumo kwenye hatihati ya KUONDOKA PSG baada ya kutua kwa Cavani. ManCity na Chelsea wanategemewa kumwaga ofa.
- ManCity sasa wanamwania winga machachari
Eduardo Salvio wa Benfica kwa dau la £25.8m.
- Kiungo mshambuliaji Juan Mata (25) anawaniwa na Arsenal.
-
Marouane Fellaini (25) anapendelea zaidi kujiunga na ManUtd kuliko Arsenal kama atafanikiwa kuhama. ManUtd wanatakiwa kumwaga £40m ili kumng'oa Everton.
- Beki
Patrice Evra (32) ameweka wazi kwamba atarudi Monaco endapo Leighton Baines atasajiliwa ManUtd.
- Beki kiwango
Leighton Baines (28) wa Everton anawaniwa na ManUtd kwa dau la £15m.
- Kiungo mshambuliaji
Miguel Michu (27) sasa huenda akatua Arsenal kwa dau la £25m.
DONE DEALS (BIG NAME TRANSFERS):

REAL MADRID
- Gareth Bale (24) ametua Real Madrid kwa uhamisho wa £85.3m (REKODI YA DUNIA) kwa mkataba wa miaka 6. Atalipwa mshahara wa £300,000 kwa wiki. Kumbuka Christiano Ronaldo alisajiliwa na Real Madrid kwa dau la £80m.

MANCHESTER UNITED

- bado bado, mwenda pole hajikwai.
ARSENAL
- Kiungo
Mathieu Flamini (29) amerejea Arsenal kutoka AC Milan kwa uhamisho huru. Flamini aliichezea Arsenal mwaka 2004 - 2008.
- Mshambuliaji
Gervinho ameuzwa AS Roma ya Italia kwa bei ya £8m.
CHELSEA

- Mshambuliaji
Samuel Eto'o (32) ametua Chelsea kwa uhamisho huru kutoka Anzhi Makhachkala, kwa mkataba wa mwaka 1.
- Kiungo mshambuliaji
Willian (25) ametua kwa uhamisho wa £30m kutoka Anzhi Makhachkala ya Urusi. Mkataba miaka 5.
- Kiungo
Florent Malouda ameondoka Chelsea kwenda Trabzonspor ya Uturuki kwa mkataba wa miaka 2.
-
André Schürrle kutoka Bayer Leverkusen ametua kwa dau £18m.
-
Marco van Ginkel ametua kutoka Vitesse Arnhem kwa dau la £8m.
LIVERPOOL

- Mshambuliaji Victor Moses amehamia Liverpool kwa mkopo wa msimu mmoja.
- Beki wa kati na kushoto Mamadou Sakho (23) ametua Liverpool kwa dau la £12m kutoka PSG.
- Beki wa kati Tiago Ilori (20) ametua Liverpool kutoka Sporting Lisbon kwa dau la £7m.
- mshambuliaji
Iago Aspas ametua kutoka Celta Vigo kwa dau la £7m.
- Golikipa Simon Mignolet ametua kutoka Sunderland kwa dau la £9m.
- Beki
Kolo Toure (32) ametua Liverpool kuimarisha safu ya ulinzi baada ya Jamie Carragher kustaafu.
- Kipa Pepe Reina ameondoka Liverpool na kutua Napoli kwa mkopo. Anaungana tena na kocha Rafa Benitez.
- Mshambuliaji kinda
Jonjo Shelvey ameondoka Liverpool kwenda Swansea kwa dau la £5m.
- Mshambulaji Andy Carroll amehamia West Ham kwa dau la £15.5m
MANCHESTER CITY
- Beki
Martin Demichelis (32) ametua ManCity kwa dau la £3.5m kutoka Atletico Madrid.
- Mshambuliaji
Stevan Jovetic (23) ametua kwa dau la £22m kutoka Fiorentina.
- Mshambuliaji
Alvaro Negredo (27) ametua kutoka Sevilla kwa dau £20m.
- Beki
Maicon (31) ameondoka ManCity kwenda AS Roma, baada ya kucheza mechi 13 tu tangu ajiunge na City.
-
Fernandinho ametua kutoka Shakhtar Donetsk kwa dau la £30m.
-
Jesús Navas ametua kutoka Sevilla kwa dau la £16m.k


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo