JOYCE KIRIA AMUIBUA MTOTO ALIYEOLEWA AKIWA NA MIAKA 8 TU

Kesho jnne katika kipindi cha ''Joyce Kiria Wanawake Live'' utapata kuona binti ambae huena akavunja rekodi ya kuolewa akiwa mdogo, ambae aliolewa akiwa na miaka 8 tu. Haya ni maisha wanayopitia watoto wa kike kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu.  usikose kutazama Wanawake Live kesho saa 3 kamili usiku EATV.
 
chini ya hizi picha kuna video fupi ya huyu mtoto akielezea mkasa huo...

NILIPOMFUATA KISIMANI NILITEGEMEA KUSIKIA HABARI ZA SHULE, kumbe LOH???!!! ni mke wa mtu kwa miaka 4 sasa

Huyu ndio Happy ambaye aliolewa akiwa na miaka 8 tu. na ameshakaa kwa mume miaka minne. alikuwa anachota maji ya kufulia

Huyo ndo Mume wa Happy anaitwa Samson. hapa nikijua ni mzazi wa Happy, Kumbe!! Mtumeeeee
Aliyevaa nguo nyekundu ni mke mwenzake na Happy, mke mkubwa wa mwanaume aliyemuoa Happy. nae utamsikia katika kipindi cha ''Joyce Kiria Wanawakelive''

Nikiwa na Mwanaharakati kutoka TAMWA Valeria, ambaye ameongelea mchakato wa rasimu ya katiba inamsaidiaje mtoto kwa haki zake.
katika kipindi cha Joyce Kiria Wanawake Live Jumanne hii tarehe 3 September 2013, utaona kwa urefu mwanzo mwisho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo