TATIZO LA MAJI NJOMBE, WANAFUNZI WAKIONA CHA MTEMA KUNI


Jumla ya Wanafunzi 84 wanatarajia Kufanya Mitihani yao ya Kuhitimu Darasa la Saba Katika shule ya Msingi ya St.Benedict Iliyoko Ramadhani Mjini Njombe.
=============

Adha ya Maji Katika Mkoa wa Njombe Imetajwa Kuwa Kikwazo hadi kwenye Sekta ya Elimu Kutokana na Wanafunzi wengi Kutumia Muda Mwingi Kutafuta Maji Badala ya Masomo

Tatizo Hilo la huduma maji  Mkoani Hapa  Limeendelea  kuwa changa moto kubwa kwa shule nyingi   za msingi  na sekondari  hali inayo pelekea wanafunzi kutumia Muda Mwingi kutafuta maji katika maeneo Ya Mbali na  Mazingira ya shule.

Hayo Yamebainishwa na Makamu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Benedict Bw Flaviani Mligo Iliyoko Ramadhani Mjini Njombe  wakati wa MaHafali ya 11 ya darasa la
saba Agosti 31 Mwaka Huu shuleni hapo ambapo makamu mkuu huyo amesema licha ya shule hiyo kuwa na mabomba lakini Wanalazimika kufuata maji mtoni na visima vya mitaani

Risala ya Wanafunzi Mbele  ya Mgeni rasmi Bwana Shejamabu Kutoka Kampuni ya Tanwatt Kibena Imeeleza  Kuwa Licha Adha ya Maji na Changamoto Mbalimbali wanazokabliana nazo Lakini watahakikisha wanafanya Vizuri Katika Mitihani yao ya Kuhitimu Darasa la Saba Inayotarajia Kufanyika September 10 na 11 mwezi huu.

Kwa upande wao wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo wamewashukuru walimu kwa kuwalea na kuwafundisha huku wakiahidi kuendelea kuwasomesha mpaka elimu ya juu.

Jumla ya Wanafunzi 84 wa Darasa la Saba wanataraji Kufanya Mtihani huo Mwaka Huu Katika Shule Hiyo ya St.Benedict Ambapo Pamoja na Mambo Mengi Uongozi wa Shule Hiyo Umesema Big Results Now Katika Sekta ya Elimu Inahitajika Kuboreshwa Katika Shule zote Bila Kubagua.
 Na Prosper Mfugale Njombe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo