MAPOKEZI YA
MWENGE WA UHURU KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Ndugu
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Napenda
nitumie fursa hii kuwafahamisha wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Mwenge wa
Uhuru utawasili Mkoani kwetu kesho
tarehe 04/09/2013 ukitokea Mkoa wa Pwani na makabidhiano rasmi yatafanyika pale
Airport Terminal 1 saa 3:00 asubuhi. Baada ya makabidhiano Mwenge wa Uhuru
utakimbizwa katika wilaya zote tatu kama ifuatavyo;-
1.Tarehe
04/09/2013 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni.
2.Tarehe
05/09/2013 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala.
3.Tarehe
06/09/2013 utakimbizwa katika Wilaya ya Temeke.
Ndugu
Wananchi,
Mwenge
wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam utazindua, kufungua au kuweka mawe ya
Msingi katika miradi 26 yenye jumla ya thamani ya T.shs. BILIONI 23.2. Mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakuwa
katika sehemu tofauti tofauti kulingana na Wilaya husika.
Katika Wilaya ya
Kinondoni Mwenge wa Uhuru
utakesha katika SHULE YA MSINGI
BUNJU “A”. Katika Wilaya ya Ilala
Mwenge wa Uhuru utakesha katika SHULE
YA MSINGI MAJANI YA CHAI. Katika
Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utakesha katika VIWANJA VYA ZAKHEM-MBAGALA KUU.
Ndugu
Wananchi.
Ujumbe
wa Mwenge mwaka huu unasema WATANZANIA
NI WAMOJA TUSIGAWANYWE KWA MISINGI YA TOFAUTI ZETU ZA DINI, ITIKADI, RANGI NA
RASILIMALI. Ujumbe huu
umeandaliwa kwa mwaka huu ili kutoa msisitizo juu ya umuhimu wa kuimarisha
Umoja na Amani katika jamii yetu.
Sambamba na ujumbe huu suala la
Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar litafafanuliwa kwa kuzingatia umuhimu wake katika kuenzi historia na
maendeleo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia mapambano dhidi ya UKIMWI,
Rushwa na Matumizi ya Dawa za kulevya yataendelea kusisitizwa. Ujumbe huu utatolewa katika maeneo
mbalimbali katika Wilaya zote tatu hususani katika mkesha wa Mwenge.
Ndugu
Wananchi,
Kila
eneo ambalo Mwenge umepangiwa kuzindua miradi au kuweka mawe ya msingi
patatolewa ujumbe mahsusi wa Mwenge na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu
Juma Ali Simai kama ilivyo
desturi nawaomba mjitokeze kwa wingi kuulaki Mwenge wetu wa Uhuru katika maeneo
yote.
Ndugu
Wananchi,
Mwenge
wa Uhuru utamaliza mbio zake hapa Mkoani tarehe 07/09/2013 na utakabidhiwa kwa
uongozi wa Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ndege wa Kilwa Masoko saa 3:00
asubuhi.
Ndugu
Wananchi,
Napenda
nitoe wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuupokea
Mwenge wetu wa Uhuru kama ilivyo desturi yetu kwa Utulivu, Amani, Umoja na
Mshikamano na kushiriki kikamilifu katika maeneo yote tuliyopanga kuzindua
miradi na kuweka mawe ya msingi.
IMETOLEWA NA
Saidi
Meck Sadiki
Mkuu
wa Mkoa
DAR
ES SALAAM
03/09/2013

