SHULE YA MSINGI NTULYA YA JIJINI MWANZA YAZINDULIWA NA RAIS KIKWETE

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwanzilishi na Mkurugenzi waShirika la Africa School House Bi.Ainee Bessire (watatu kushoto) pamoja naMbunge wa Misungwi Charles Kitwangwa(kushoto) na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi shule ya msingi Ntulya katika kata ya Mondo wilayani Misungwi.Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Ntulya muda mfupi baada ya kuizindua katika kata ya Mondo wilayani Misungwi Jana. Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo. 
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo