SERIKALI YAHAKIKISHIA UMMA KUWEPO KWA WATAALAMU WA KUTOSHA WA AFYA


Rais  Jakaya  Kikwete  amesema  serikali  yake   itaendelea    kuhakisha  kuwa   kuna  kuwepo  na wataalamu  wa kutosha  katika  vituo  vya   afya  hasa  maeneo  ya  vijinini  ambapo  changamoto  hiyo  ni kubwa  kuliko  mijini.
 
Mh  kikwete   ameyasema  hayo  alipokuwa   akifugua  mkutano  wawafanyakazi  na  wadau  mbalimbali katika   sekta  hiyo uliondaliwa  na  taasisi   ya   Benjamin   Mkapa 

Naye   waziri  wa  afya  na  ustawi  wa jamii  Mh  Dk Hussein  Mwinyi  amesema  katika kuhakikisha  kuwa huduma   za  afya zinakuwa bora  serikali  imejipanga kuona kuwa vituo vyote vipya vya afya  vinapatiwa wafanyakazi ili huduma ziweze  kuwafikia watu wengi  zaidi

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na  rais mstaafu Mh Benjamini Mkapa ambaye ndiye mwasisi wa  taasisi hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi   Mtendaji  wa  taasisi hiyo  ya  Mkapa  Dk Hellen  Senkoro  amesema   wamejipanga vyema kuhakisha  wanakabilina na changamoto za mabadiliko ya upatiknai wa misada mkutoka kwa wafadhili mbalimbali kutokana na mtikisiko wa uchumi uliotokea kipindi cha  nyuma


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo