Jeshi
la polisi kanda maalum ya Dar es salam limemkamata Saida Mohamed huko
Kigamboni akiwa na sare mbalimbali za jeshi la wananchi.
Kamishna
wa kanda hiyo Suleiman Kova amesema katika tukio lingine jeshi hilo
limefanikiwa kuzima jaribio la wizi katika kampuni ya fast jet baada ya
kunasa mawasiliano ya mtandao wa majambazi na baadhi ya wafanyakazi wa
kampuni hiyo