Habari zilizotufikia punde kutoka vyanzo vyetu vya habari ni kwamba
mchungaji Raphael Seleli wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G)
Kinyerezi jijini Dar es salaam amefariki dunia hospitalini
jijini hapa baada ya kusumbuliwa ugonjwa wa ini kwa kipindi cha
takribani miezi mitatu sasa ambapo alipelekwa nchini India kwa matibabu
kisha kurejeshwa nchini na kuendelea na matibabu mpaka kifo kilipomkuta
jioni ya Jana.
Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
chanzo: gk blog
