Mbunge
wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akimpatia tiketi ya ndege
na nyaraka zinginezo, Nuru Sinna ambaye ametimiza vigezo kwenda kufanya
kazi Dubai, Falme za Kiarabu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam
hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Jaffari Kingwande (wa pili kulia)
ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bravo Job Centre iliyofanikisha
kupata kazi hiyo pamoja wengine wengi watakaokwenda siku za usoni.Wa
pili kushoto ni Mohamed Omari Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo.
Mtemvu
akionesha nyaraka ikiwemo viza, vibali vya kazi pamoja na tiketi ya
Nuru Sunna kwenda Dubai. Jaffari Kingwande (wa pili kulia) ambaye ni
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bravo Job Centre iliyofanikisha kupata
kazi hiyokufanyakazi.
Mtemvu
akizungumza katika mkuta na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu
changamoto mbalimbali ambazo anazipata katika jitihada zake za
kuwatafutia kazi watanzania Falme za Kiarabu. Alisema kuwa baadhi ya
maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwemo
Waziri Belnald Membe wanashiriki kukwamisha jitihada hizo.
Mtemvu (mbele katikati) akiwa katika hafla hiyo.
Nuru Sunna (kushoto) akiwa na mdogo wake katika hafla hiyo.