Mbio za Mwenge zilipiga kambi katika Wilaya ya Temeke kwenye Viwanja
vya Mbagala Zakhem jijini Dar hapo jana Septemba 6 mwaka huu, ambapo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na mwenyeji wake Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Bi. Sofia Mgema walihudhuria mapokezi hayo.
Pia viongozi mbalimbali wa serikali, watumishi wa umma na wananchi
kutoka sehemu tofauti hapa jijini Dar kwa pamoja waliupokea Mwenge huo
na kushiriki michezo iliyoandaliwa kwa niaba ya kiongozi wa mbio za
Mwenge kwa mwaka huu, Juma Ali Simwai. Kauli mbiu ikiwa ni:
“Watanzania ni wamoja tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasilimali.”
(PICHA NA CHANDE ABDALLAH NA DENIS MTIMA/ GPL)