Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuashiria kuzindua Benki mpya ya UBL, iliyopo Mtaa wa
Samora jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo
iliyofanyika leo Sept 4, 2013. Kushoto na kulia kwa Makamu wa ni baadhi
ya viongozi wa juu wa benki hiyo, Anwar Pervez na Atif Bakhari.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa benki ya UBL iliyozinduliwa
leo Sept 4, 2013 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya UBL, Zamees Ghudrey, akizungumza wakati alitoa
shukrani baada ya uzinduzi huo, uliofanyika leo Sept 4, 2013.
Baadhi
ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa benki hiyo, wakimsikiliza Makamu
wa Rais , wakati alipokuwa akiwahutubia kwenye uzinduzi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata Keki maalum iliyoandaliwa kuashiria uzinduzi wa benki hiyo mpya
ya UBL, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika leo Sept 4, 2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki mpya
ya UBL, baada ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika leo, jijini Dar es
Salaam. Picha na OMR.