KAMPENI YA TUPO WANGAPI ? TULIZANA AWAMU YA PILI YAZINDULIWA, WANAHABARI WAPONGEZWA KWA MCHANGO WAO



 Mganga  mkuu  wa  serikali  Dr  Donan Mmbando  akifungua  kampeni ya awamu ya  pili ya Tupo  wangapi ? Tulizana  
............
MGANGA  mkuu  wa  serikali  Dr  Donan   Mmbando  amevipongeza  vyombo  vya habari  nchini Tanzania  kwa jitihada  kubwa  za  kuelimisha  jamii  kupitia kampeni ya Tupo  wangapi?  TULIZANA  awamu ya  kwanza.

Dr Mmbando  ametoa  pongezi  hizo  leo  jijini Dar  es Salaam  wakati  wa  ufunguzi  wa awamu ya  pili  ya kampeni ya  TUPO WANGAPI? TULIZANA awamu ya  pili.

Mbali ya  pongezi  hizo  bado ametaka  wanahabari  nchini  kuendelea kutoa  ushirikiano  katika  kuelimisha  jamii  dhidi ya  kampeni   hiyo.

Alisema  kuwa tafiti  zinaonyesha  kuwa  mahusiano  ya  kingono  kwa  kuwa  na  wapenzi  wengi ni chanzo  kikuu cha VVU

Kwani  alisema asilimia  zaidi ya  24  watu  waliopo katika ndoo  wamekili  kuwa  na mahusiano ya  kingono asilimia 4 ya  wanawake  waliopo katika  ndoa wamekili  kuwa na mahusiano  ya  mpenzi  zaidi  ya   mmoja
 
Alisema upo  uwezekano  wa  mtandao  wa  ngono  kuendelea  kukuwa  zaidi  iwapo  watu  hawatatulizana  kwa  kuwa na  mpenzi mmoja  ambae ni mwaminifu.

Matokeo ya  utafiti  wa  viashiria  vya malaria na  UKIMWi  vinaonyesha  kuwa  kasi  ya  maambukizi  ya  VVU  ni  kubwa  zaidi  kwa  kuwa na asilimia 5.5

Upo  uwezekano  wa  kupunguza maambukizi ya VVU  kwa  kutulizana  kwa  kuwa na  mpenzi  mmoja  mwaminifu .

Awamu  ya  kwanza na kampeni   hii  imeonyesha mafanikio  makubwa  baada ya  wasanii kutunga  nyimbo mbali mbali  pia  taasisi  mbali mbali  zimepata  kuweka mabango  na vielelezo mbali mbali  vinavyohamasisha  jamii  kuepuka na mtandao  wa  ngono.

“Utafiti  wa  kufuatilia  mwenendo  wa kampeni  hizo  umeonyesha  asilimia 71 wamekili  kuona  jitihada  hizo  hivyo  awamu ya  pili  wizara  ya  afya na ustawi wa jamii  imepania  kuongeza kasi  zaidi ikiwa ni  pamoja na kutumia  vyombo  mbali mbali  vya habari..tunapenda  kupongeza  wanahabari  nchini  kutokana na  kuendelea  kutoa elimu kwa  jamii  hivyo  ni mategemeo yetu  kuendelea  kuelimisha  zaidi jamii.”

Dr Mmbando  alisema serikali  itaendelea  kubuni  mbinu  mbali mbali  za  kuelimisha jamii  juu ya kampeni  hii  bila  kuwatisha  wananchi .

Pia  alisema  kuwa kampeni  hii  serikali  itahakikisha  inawafikia  wananchi  wote  hata  wale  waliopo  pembezoni  kwa ngazi ya  wilaya  hadi  kijiji huku  akisisitiza  kuwa  magari  ya  sinema  ambayo  yapo  wilayani  yatatumika kutoa  elimu  zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo