Katibu mkuu wa Tanzania Professional Boxing Organisation (TPBO) Ibrahim Kamwe ambaye anajulikana kwa jina la bigright amejitoa katika uongozi wa chama cha ngumi kama kiongozi.
Bigright
ambae ukiondoa mambo ya kichama mara nyingi amekuwa akiwaongoza maofisa
wa chama hicho katika shughuli mbalimbali na mapambano mengi kama jaji
mkuu,muhifadhi rekodi za mabondia na mshauri katika shughuli za
kiufundi.
Akizungumza
na vyanzo vya habari amesema ameamua kupumzika shughuli za TPBO na
kurudi kwenye ufundishaji wa vijana na kuendelea na kampuni yake ndogo
ya bigright promotion ambayo inajihusisha na utayarishaji wa matamasha
na uandaaji wa mapambano ya ngumi. ‘ kwa kuwa naupenda mchezo wa
ngumi nimefanya shughuli hii kwa muda mrefu kukiwa na utatautata wa
hapa na pale na yote hii kwa ajili ya kuuendeleza mchezo wa ngumi
nchini lakini imekuwa ni ngumu kwangu kuendelea na wadhifa huo ,
nawashukuru maofisa wenzangu wamekuwa wakinipa ushirikiano wa karibu.
Ila kwa sasa najitoa katika uongozi na nitajihusisha na ngumi kivingine
ikiwemo kuwaendeleza vijana na kuandaa mapambano madogomadogo ya kukuza
vipaji.
