ALIYEMWIBIA MKUU WA MKOA WA NJOMBE ATUPWA JELA MWAKA MMOJA

Mahakama ya Wilaya ya Njombe Jana  Imemuhukumu Kifungo cha Mwaka Mmoja Jela Izack Kahogo Mkazi wa Kambarage Mjini  Njombe  Baada ya Kumkuta na Kosa la Wizi Katika Nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kaptein Mstaafu Aseri Msangi.

Akisoma Hukumu Hiyo Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Amesema Mahakama   Imetoa Adhabu Hiyo Kwa Mshtakiwa Chini ya Kifungu cha Sheria Namba 258 Kifungu Kidogo cha Sheria Namba 256 Sura ya 16 Kilichofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002,Pamoja na Kuridhishwa na Ushahidi Uliotolewa na Upande wa Mashtaka.

Ameongeza Kuwa Mahakama Imetoa Adhabu Hiyo  Kwa Kuzingatia Utetezi na Ombi la Mshtakiwa ya Kuomba Apunguziwe Adhabu Kwani Amekaa Mahabusu Kwa Takribani Mwaka Mmoja.

Awali Akisoma Hati ya Mashtaka Mwendesha Mashtaka  Selapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Mshtakiwa Alitenda Kosa Hilo  selaphiani Agosti 26 Mwaka Jana  na Kwamba Alifikishwa Mahakani  29 Agosti Mwaka 2012.  

Imedaiwa Mahakamani Hapo na Mwendesha Mashataka Kuwa Siku ya Tukio Mshtakiwa Alifika Nyumbani Kwa Mkuu wa

Mkoa wa Njombe na Kuiba Kompyuta Ndogo  LAPTOP Aina ya Lanovo na Simu Tatu Zenye Thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili.

Wakati Huo Huo Mahakama Hiyo Imemuhukumu Kifungo cha Miezi Sita Jela Ama Kulipa Faini ya Shilingi Elfu  30 Winfirida Wilomo Mkazi wa Kifanya Wilaya ya Wanging'ombe Baada ya Kumkuta na Hatia ya Kujifungua na Kumtupa Mtoto Mchanga wa Siku Moja Chooni na Kusababisha Kifo cha Kichanga Huyo.

Akitoa Hukumu Hiyo Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Amesema Mahakama Imetoa Adhabu Hiyo Chini ya Kifungu cha Sheri Namba 218 Kifungu cha 35 cha Kanuni ya Adhabu , Sura ya 16 Kilichofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002.

Hakimu Kapokolo Ameongeza Kuwa Mahakama Hiyo Imetoa Adhabu Hiyo Kwa Kuzingatia Utetezi na Maombi ya Mshtakiwa Kuwa Alikuwa na Mtoto Mdogo Mwenye Umri wa Mwaka Mmoja.

Awali Akisoma Hati ya Mashtaka Mwendesha Mashtaka Selapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Mshtakiwa Alitenda Kosa Hilo Agosti 19 Mwaka Huu Majira ya Saa Sita Usiku na Kwamba Alikamatwa Agosti 23 Mwaka 2013 na Kuongeza Kuwa Mshatakiwa Amefikishwa Hii Leo Kwa Mara ya Kwanza na Kusomewa Hukumu Baada ya Kukiri Kutenda Kosa Hilo.

Akitoa Utetezi Wake Mahakamani Hapo Mshtakiwa Ameiambia Mahakama Kuwa Alifanya Hivyo Kutokana na Kichanga Hicho Kutoonesha Dalili za Kuwa Hai na Kwamba Alikuwa na Mtoto Mdogo wa Mwaka Mmoja.

NA GABRIEL KILAMLYA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo