Watu
wawili wamefariki dunia na kumi wamejeruhiwa baada ya gari aina ya
pickup mali ya kampuni ya Hood iliyokuwa imebeba ndugu wa familia moja
wakielekea msibani kuacha njia na kupinduka mara tatu katika eneo la
kata ya mkuyuni wilayani morogoro.
Vilio na majonzi vilitawala katika hospitali ya mkoa wa Morogoro mara baada maiti na majeruhi kuwasili
Ambapo
ndugu wa marehemu wamesema waliofariki ni Leila Ngurungu pamoja na
kaka yake aliyekuwa mchezaji wa siku nyingi katika soka Idrisa Ngurugu
ambapo wamesema walikua njiani kwenda kwenye msiba wa kaka yao mkubwa
ambapo njiani walipata ajali na kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi
huku baadhi wa ndugu wakieleza kuwa msiba huo ni pigo kwani wamepoteza
ndugu watatu wa familia moja.
Nao
majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa morogoro
wakiziungumzia tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni dereva wa gari
aina ya pickup aliekua akijaribu kukwepa ajali ya uso kwa uso na kisha
gari kuacha njia na kupinduka mara nne.
Jeshi
la polisi Mkoa wa morogoro limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na
maiti zimehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa
morogoro na majeruhi wanaendelea na matibabu