WATU 27 WAUAWA NA FISI MKOANI GEITA NA MWANZA

WATU 27 Wameuawa na fisi katika matukio tofuati kwenye mikoa ya Geita na Mwanza katika kipindi cha mwaka 2012 /2013na wengine saba kujeruhiwa.

Hatua hiyo imedaiwa kuitisha serkali kutokana na kupotea kwa nguvu kazi kwani wengi wa wailiouawa ni watoto na tayari Kikosi cha nguvu kazi kimepelekwa kanda ya ziwa kutoa elimu juu ya tabia ya fisi kwa kutumia sinema na kuwasaka fisi hao.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii imefafanua kuwa pia fisi 33nao  wameuawa na kikosi cha kukabiliana na ujangili kanda ya mwanza lakini kikwazo kikubwa cha utekelezaji zoezi hilo ni kukosa ushirikiano kutoka kwa jamii kutokana na kuamini kuwa fisi hao wanafugwa kichawi.

Kikosi hicho cha nguvu kazi kilichoaza zoezi hilo Agosti 16 mkoani Mwanza kinaongozwa na Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Umma wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bwana Twaha Twaibu akisaidiwa na Bwana Benjamini Kijika Mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangiri kanda ya ziwa.

Katika utekeelzaji huo wa kutoa elimu kwa jamii katika maeneo yaliyoathiriwa na wimbi la mauaji ya fisi elimu itatolewa kupitia nadharia na sinema hata hivyo Mkoa wa Geita ndio ulioathirika zaidi ikilinganishwa na mikoa ya Mwanza na Simiyu na Shinyanga.

Akizungumzia hali hiyo mara baada ya kuanza ziara ya kikaziya siku tano  Mkoani Geita juzi   Mkuu wa idara ya Elimu kwa Umma wa Wizara ya Maliasili na utalii Bwana Twaha Twaibu jana amesema kuwa hadi june 2013 familia 93 zilikuwa zimelipwa kifuta machozi cha shilingi milioni 49 kwa nchi nzima katika matukio yanayotokana na wanyama wakaliwakiwemo fisi kuua binadamu.

Kwa mujibu wa sheria wanachi pia wameelezwa kuwa mtu anapouaw a na mnyama familia yake ina haki ya kulipwa kifuta machozi cha shilingi milioni MOJA,na aliyejeruhiwa na kuachwa na kilema cha kudumu ni shilingi Lakitatu na  jeraha la kawaida n shilingi Lakimbili na kuachana na imani potofu kuyahusisha na ushirikina.

Tatizo la kukabiliana na  mauaji yanayofanywa na fisi katika mikoa ya kanda ya ziwa limekuwana  changamoto kubwa kutokana na  jamii ..kuyahusisha matukio hayo na imani za kishirikina na hivyo jamii kutokuwa tayari kutoa ushirikiano katika kuwasaka na kuwaua fisi wakihofia kudhurika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo