Katika msako mkali uliodumu masaa matatu, polisi
walinasa wanaume hao wengi wao wanafunzi wa vyuo vilivyo eneo hilo,
baada ya wafanyabiashara mjini humo kulalamika kwamba ukahaba umezidi.
OCPD wa Thika Paul Letting alisema wengi wa wanaume
hao watafikishwa kortini kujibu mashtaka ya kurandaranda wakiwa na lengo
la kuuza ngono.
Alisema maafisa wa polisi wameweka mikakati ya kufagia
makahaba wote Thika ambao alisema wameongezeka kutokana na kukamilika
kwa barabara kuu ya kutoka Thika kuelekea Nairobi.
Msemaji wa Wauzaji Ngono eneo hilo Barrack Ondiek
alithibitisha kwamba wakahaba wa kiume wameongezeka sana mjini humo
katika kipindi cha miezi sita iliyopita baadhi wakiwa wametoka Mombasa,
Mlolongo na Nairobi.
Alisema kati ya 45 waliokamatwa, 10 ni wa kutoka
Thika. Wengine ni wanafunzi wa chuo kikuu kimoja ambao Jumanne
walifikishwa kortini Thika na wakaachiliwa huru kwa dhamana.
Alifichua kuwa ushoga unaenea sana Thika kutokana na
kusajiliwa kwa Chama cha Mashoga mjini humo miezi mitatu iliyopita na
sasa chama hicho kina wanachama zaidi ya 200.