SHAHIDI ATUPWA RUMANDE KWA KUTOA USHAHIDI WA UONGO MAHAKAMANI

Ali Hassan Joho
Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.
 



Na GALGALO BOCHA na EUNICE MACHUHI.
SHAHIDI aliyejitokeza kutoa ushahidi katika kesi dhidi ya Gavana wa Mombasa, Hassan Joho Jumatatu ya wiki hii alijikuta pabaya alipowekwa rumande kwa kutoa ushahidi potofu licha ya kuapa na kusimama kizimbani.
Bi Zainab Said alitoa ushahidi kwamba alishuhudia kisa cha utoaji rushwa kwa wapiga kura katika kituo cha upigaji kura cha Jamvi la Wazee huko Kisauni.

Kilichomtia matatani zaidi ni alipoeleza mahakama aliripoti kisa hicho kwa msimamizi wa kike kituo hapo licha ya stakabadhi za mahakama kuonyesha kwamba afisa huyo ni mwanamume.

Hata baada ya Jaji Fred Ochieng kumtaka kutazama stakabadhi ya mahakama iliyoonyesha wazi afisi huyo ni mwanamume, Bi Said alisisitiza kwamba afisi huyo alikuwa ni mwanamke.
 
Jaji Ochieng aliagiza shahidi huyo kutiwa nguvuni na kuwekwa rumande punde tu alipoteremka kutoka kizimbani baada ya kutoa ushahidi wake.

“Nina uhahika alikuwa ni mwanamke,” akaeleza Bi Said.
Shahidi alikuwa ni miongoni mwa mashahidi watatu wa Bw Shahbal waliotoa ushahidi katika kesi ambapo anataka mahakama ibatilishe uchaguzi wa Bw Joho kama gavana wa Mombasa.

Ubishi
Jaji Ochieng alitoa agizo hilo baada ya kutilia shaka ushahidi wa Bi Said ambaye alikuwa ubishi mwingi kusisitizia mahakama kwamba afisa huyo ni mwanamke. 
 
Baadaye Jumatatu jioni Mahakama ilielezwa kwamba tayari polisi wameandika taarifa kutoka kwake na kupewa agizo la kufika mahakamani baada ya siku nne.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo