MWIGIZAJI Nyota na muongozaji bora wa filamu Swahilihood Vincent
Kigosi ‘Ray the Greatest’ amemwagiwa sifa nyingi na mwigizaji wa kike
Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ msanii huyo amedai kuwa Ray kupitia kampuni yake
ya RJ Company ltd imekuwa ikiibua vipaji vipya kila siku na kutoa fursa
kwa waigizaji chipukizi na kuigiza katika filamu zinazoandaliwa na
kampuni hiyo
Akiongea na FC mwanadada huyo amesema kuwa Ray kutokana na umahiri wake wa uongozaji bora anatumia muda mwingi katika kukuza vipaji vya wasanii ambao hawajawahi kupata nafasi kabisa ya kuigiza na kunyimwa nafasi kabisa kwa wasanii wengine wenye majina katika tasnia ya filamu lakini hali kwa Ray ni tofauti.
“Siri nampenda sana Ray kwa juhudi zake anazofanya katika kuwachukua wasanii chipukizi ambao hawana kabisa connection na wasanii wakubwa, bila shaka ni ukweli usiofichika unapoanza katika uigizaji lazima ubebwe lakini kuna wasanii wengine hawana muda huo, Ray ni mfano wa kuigwa na anastahili pongeza sana kwa moyo wake,”anasema Batuli.
.
Batuli alitolia mfano kwa Miss Tanzania wa mwaka jana Salha Isael na kuwa mwigizaji kinara katika filamu ya Bad Luck kitu ambacho kwa watayarishaji wengine isingekuwa rahisi kumwamini msanii mpya, sifa anazopewa Ray kiukwelia anastahili kwani mtayarishaji huyu amekuwa mbele sana katika kutoa mchango wake katika harakati za ukuzaji wa filamu Swahilihood BIG UP RAY KWA JUHUDI ZAKO.
Na FC