POLISI WAKAMATA MAGUNIA 20 YA BANGI MKOANI KILIMANJARO


JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, limekamata madawa ya kulevya aina ya bangi magunia 20 katika eneo la Ngare Nairobi wilaya ya Siha mkoani hapa ambako ni mpakani mwa nchi ya Kenya na Tanzania.

Mbali na magunia hayo jeshi hilo pia linamshikilia  mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Jackson Arold (19) kwa tuhuma za  kukutwa na misokoto 250 ya Bangi.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema Magunia hayo yalikamatwa Julai 31 mwaka huu majira ya saa kumi na nusu alfajiri katika kijiji cha Ngare Nairobi mpakani mwa Kenya na Tanzania, yakiwa yamepakiwa kwenye  gari lenye namba za usajili T.977 ACB aina ya Land Rover.

Kamanda Boaz alisema magunia hayo ya Bangi yalikamatwa na askari wa usalama barabarani ambapo baada ya kuliona gari na kulishtukia walilisimamisha na baada ya kusimama watuhumiwa waliokuwa na gari hiyo walitoka na kukimbia kusiko julikana na kulitelekeza gari hilo.

Inaelezwa kuwa kuwa Gari hilo lilikuwa likielekea nchi jirani ya Kenya ambako inadaiwa kuna Biashara nzuri ya Madawa hayo ya Kulevya aina ya Bangi.

Akielezea tukio la pili kamanda Boaz alisema misokoto hiyo iliyokuwa kwenye begi la mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Jackson Arold (19), ambaye ni mkazi wa Mbokomu ilikamatwa Julai 30 mwaka huu katika eneo la Kiboriloni.

Kamanda Boaz alisema  kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo lilitokana na taarifa zilizotolewa na  Raia wema  baada ya kutilia mashaka begi ambalo alikuwa amelibeba mtuhumiwa huyo.

Aidha kamanda aliongeza kuwa  jeshi lake limejiimarisha katika ulinzi hasa katika maeneo ya mipaka ili kuweza kuzuia kuingizwa na kutolewa kwa madawa ya kulevya ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni moja ya mikakati ya kutokomeza biashara hiyo katika mkoa huo na taifa kwa ujumla.

CHANZO:http://kilimanjaro-yetu.blogspot.com/2013/08/polisi-kilimanjaro-wakamata-magunia-20.html#.UfzebMX0nIV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo