MWAKYEMBE AAGIZA MATREKTA YOTE YANAYOBEBA MIZIGO BANDARINI YAENDE KWENYE KILIMO

Serikali imepiga marufuku matrekta yote yanayotumika kubeba mizigo bandari yaende yanakohitajika  kwenye kilimo na siyo kufanya kazi mjini kubeba mizigo bandari kulandalanda hovyo mijini.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa uchukuzi Dr Harson Mwakyembe  Mjini  Mbeya  wakati akiwahutubia wakazi wa mikoa ya Nyanda zajuu kusini kwenye ufunfunzi wa Maonesho ya Wakulima Nanenane yaliyofunguliwa juzi kwenye viwanja vya maonesho vya John Mwakangale Uyole Jijini Mbeya.

Dr Mwakyembe  amesema Serikali imeweza  kufuta ushuru wa zana za kilimo kama matreka  chini ya Kampeni ya Kilimo Kwanza,lakini matrekta mengi yaliyoingizwa kuwezesha kilimo kukua yameishia kubeba mizigo bandarini na kufanya shughuli nyingine nje ya sekta za kilimo.
 “Hili hatuwezi kulivumilia kwani linavunja malengo ya Serikali ya kujitoshereza kwenye kilimo,matrekta mengi  nimeyaona bandarini yakitumika kubeba kubeba mizigo, kwa mfano makontena,natoa miezi mitatu kuanzia sasa matrekta yote yanayotumika bandarini yaende yanakohitajika kwenye kilimo,Ikifika Oktoba 30 mwaka huu matrekta yatakuwa marufuku kuingia bandarini.”Alisema Dr Mwakyembe.

“Nitaongea na Uongozi wa Sumatra na Polisi kupiga marufuku matrekta yasionekane Mijini badala yake yaende mashambani kulima na kubeba mizigo  huko .”

Katika hatua nyingine amezishukia Halmashauri  kwa kusema kuwa wakati juhudi zikiendelea za serikali ameziagiza Halamsahuri zote kuondoa kero zianzowakatisha tamaa wakulima  kero zinazozalisha mazingira hasi, mazingira yasiyo wezeshi.

Akitolea mifano kodi za kukera ambazo zinaendelea kutozwa ndani ya wilaya kumbana mkilima anayetoa mazao yake shambani kwenda nyumbani au kwenda gulioni zinawakera sana wakulima.

Alisema kwa kuwa Halmashauri zimejaa wataalam wenye ujuzi mbalimbali amewahimiza kuttumia weledi na elimu yao kubuni njia mpya zisizokera wananchi za kuongeza mapato ya Halmashauri zao kuliko kuwaera wakulima wanaojitafutia kujikwamua kuondokana na umasikini kwa kuwaongezea kera.

Akizungumzia kuwawezesha wakulima kupata umeme vijijini ili kuzalisha zaidi na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa mwaka huu wa Fedha Serikali imelekeza nguvu kubwa kupeleka umeme kwa wakulima, kupitia wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Ameleza kuwa vijiji 590 vya mikoa ya Mbeya ,Katavi,Ruvuma,Rukwa,Njombe,na Iringa vimetengewa jumla ya Shilingi bilioni 162.5 kwa ajili ya umeme ambao utatekelezaji wake umeishaanza kwa kazi  kwa uteuzi  wa makandarasi  ambao wanatakiwa kuanza kazi ya usambazaji  umeme vijijini oktoba mwaka huu.

Akaongeza  kuwa miradi hii ya umeme itachochea uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo vijijini vitakavyoongeza thamani ya mazao ya wakulima,na serikali imechukua hatua ya ziada ya kupunguza gharama za kufungiwa umeme Vijijinikwa asilimia 70.

Kuhusu miradi ya barabara alieleza kuwa mbali na miradi mikubwa ya barabara inayoendelea kutekelezwa kitaifa,mikoa ya Nyanda za juu Kusini imetengewa zaidi ya Shilingi Bilioni 5 kwa kazi  ya kukarabati barabara za vijijini,alisema kiasi hiki cha pesa kikisimamiwa vizuri kitaleta mabadiliko katika kusafirisha mazao vijijini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Aser Msengi akimkaribisha Waziri wa Uchukuzi Dr Harson Mwakyembe  kukamilika kwa  Kiwanja  cha Ndege  cha Kimataifa cha  Songwe  kitawezesha wananchi wa mikoa ya nyanda za juu Kusini kusafirisha mazao yao moja kwamoja kwenda kwenye masoko ya nje na wao kutolazimika kupitia kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu  Nyerere na cha Kilimanjaro kwenda ughaibuni.

Awali katika Salaam za TASO wakati wa Uzinduzi rasmi wa Sherehe  ya sikukuu ya wakulima na Maonesho ya Kilimo Nanenane Kikanda Kwenye uwanja wa Maonesho ya Kilimo salamu zilizosomwa na Katibu wa TASO  Kanda ya Nyanda za Juu  Kusini Ramadhani Kiboko  badala ya Mwenyekiti wa Taso Kanda Kapt. Mstaafu Zeno Noel Nkoswe, alitoa wito kwa wananchi wa Kaanda ya Nyanda za juu Kusini na wakazi wa Jiji la Mbeya na Vitongoji vyake  kujitokeza kwa wingi  kuja  kujionea maonesho yaliyosheheni teknolojia mbalimbali katika kilimo, mifugo,uvuvi, na ushirika kwa siku zote za maonesho ya mwaka huu, yanayolenga kukidhi matakwa ya kaulimbiu ya ya Nanenane 2013isemayo ZALISHA MAZAO YA KILIMO NA MIFUGO KWA MAHITAJI YA SOKO.

Akaeleza kuwa kwenye maonesho hayokuna jumla ya washiriki 399 kati ya waalikwa 387 wapo tayari mabandani wamepanga bidhaa zao za maonesho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo