Mtuhumiwa Fredrick Ngailo baada ya kushushiwa kipigo.
Wimbi la wizi majumbani mwa watu linaloendelea kushika kasi Makete mjini limeonesha kuwakera wananchi baada ya kuamua kuchukua sheria mkononi na kumshushia kipigo kikali mtuhumiwa wa wizi aliyenaswa akifanya jaribio la kuiba
Mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fredrick Ngailo (pichani) anadaiwa kukamatwa akiwa na nyundo akivunja nyumba ya Lualua Sanga mkazi wa kona Makete mjini bila aibu majira ya saa 1 jioni
Imeelezwa kuwa baada ya jaribio hilo la wizi kushtukiwa na mke wa Lualua, mtuhumiwa huyo wa wizi alitaka kumjeruhi kwa kumpiga nyundo ya kichwa lakini katika purukushani alikwepa na nyundo hiyo kumpata mguuni, huku mwananmke huyo akiendelea kupiga mayowe yaliyowaita majirani waliofika eneo la tukio akiwemo baba mwenye nyumba aliyekuwepo kibandani kwake mbali kidogo na nyumbani
"Kweli tulishtushwa na kelele za mwizi, na tulipofika tulimkuta mtuhumiwa akiwa na nyundo mkononi huku mwanamke mwenye nyumba hii akisema walitaka kumpiga nayo baada ya kumkamata akifanya jaribio la kuvunja nyumba kwa lengo la kuiba" alisema mwanaume mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake
Mtandao huu ulishuhudia jamaa huyo akiwa amepewa kichapo cha mbwa mwizi huku wakimpeleka kituo cha polisi Makete kwa hatua za kisheria baada ya kumpiga
Akizungumza na mtandao huu akiwa amewekwa chini ya ulinzi akipelekwa kituo cha polisi makete mtuhumiwa huyo Bw. Fredrick Ngailo alikiri kwenda kwenye nyumba hiyo kwa lengo la kuiba pamoja na kufanya mapenzi na msichana mmoja anayeishi kwenye nymba hiyo ambaye ni bubu
Amesema walikubaliana mchana na ndipo alipokwenda kwa ajili ya kutekeleza ahadi hiyo na ndipo alipokamatwa kwa kuwa arobaini yake ilikuwa imefika
Hadi tunairusha habari hii mtuhumiwa huyo alikuwa anapelekwa kituo cha polisi Makete