Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linamshikilia Maria Kilasi Ambapo Anatuhumiwa Kutupa Mtoto Mchanga Ndani ya Shimo na Kisha Kumfukia na Kusababisha Kifo cha Mtoto Huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Agosti 26 Mwaka Huu Majira ya Saa Tano Asubuhi Katika Eneo la Mashujaa Mjini Makambako Baada ya Mbwa Kufukua Mwili wa Mtoto Huyo.
ACP Ngonyani Amesema Mnamo Agosti 23 Mwaka Huu Mtuhumiwa Alijifungua Mtoto wa Kiume na Siku ya Agosti 26 Mwaka Huu Alimfukia Ndani ya Shimo na Kwamba Upelelezi Dhidi ya Tukio Hilo Linaendelea, Mtuhumiwa Atafikishwa Mahakamani Pindi Upelelezi Huo Utakapokamilika.