
Na Denis Mlowe, Iringa
WATU
wawili wamefariki dunia kwa kuzama maji akiwemo mtoto Gift Kadafu (2.5)
mkazi wa kijiji cha Kitanzini Ndiwili, Wilaya ya Iringa,aliyefariki
dunia baada ya kuzama kwenye Mto Ruaha.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa tukio hilo
lilitokea Agosti 22 saa 10:00 jioni mtoto akiwa na mama yake kando kando
ya mto Ruaha.
Mungi
alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kuweza kubaini nini chanzo
kutokana na kuonekana kuna uzembe kwa mtoto huyo kuzama hadi kufariki
akiwa na wazazi jirani.
Mungi
alisema chanzo cha kifo hicho ni uzembe wa wazazi wake wa Matalawe
alikamatwa kutokana na ushirikiano mzuri baina ya jeshi la polisi na
askari wa wanyama pori wa hifadhi ya taifa ya Ruaha..
Katika
tukio jingine lililotokea maeneo ya Luhanga kata ya Nyabula wilaya ya
Iringa Fausta Mhulo (54 alifariki dunia baada ya kutumbukia kwenye
kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake.
Mungi alisema kifo hicho kilitokea majira ya saa 3 usiku chanzo cha kifo hicho ni ugonjwa wa akili aliokuwa nao marehemu .