MFANYA BIASHARA ALIYETEKWA NYARA NA WATU WASIOJULIKANA APATIKANA

Murang'a
Mashamba yaliyopandwa majani chai katika kaunti ya Murang'a. Picha Na SAMUEL KARANJA.

MFANYABIASHARA wa kaunti ya Murang’a aliyetekwa nyara akiwa kaunti jirani ya Kirinyaga amepatikana.
Kulingana na polisi, Bw Harrison Gichuhi ambaye anamiliki kituo cha mafuta ya petroli katika soko la Kagio huko Kirinyaga nchini Kenya, alipatikana siku ya Jumanne jioni.

Mfanyibishara huyo alitekwa nyara wiki jana na wakora watatu waliovalia sare za polisi.

“Alitwambia kuwa, alikuwa amefichwa kwenye nyumba moja katika kijiji cha Gikindu kaunti ya Murang’a,” alisema Bw Odede.

Baada ya kutoroka, mfanyibiashara huyo alipata usaidizi kutoka kwa majirani na kisha kupelekwa katika kituo cha polisi kuandikisha ripoti.

Watekaji nyara hao walikuwa wameitisha Sh3 milioni ili kumwachilia lakini Bw Odede alisema fedha hizo hazikulipwa.

Hata hivyo, afisa mmoja wa polisi ambaye aliomba asitajwe jina, aliambia Taifa Leo kuwa huenda ikawa familia hiyo ililipa watekaji nyara hao kitita fulani cha pesa.

Bw Gichuhi alishambuliwa na wezi hao mwendo wa saa moja jioni siku ya Alhamisi wiki jana.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, walificha gari lao karibu na kituo cha mafuta na wawili wakatoka nje huku wakitaka kumtia pingu.

Hata hivyo, alikataa kukamatwa huku akitaka kujua sababu ya kutiwa mbaroni na katika harakati hiyo, wanaume hao wawili walimtupa ndani ya gari na kutoroka naye.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo