MATUMIZI YA TINDIKALI SASA NI KWA LESENI MAALUMU

Tindikali.
Baada ya kukithiri kwa matukio ya uhalifu kwa kutumia tindikali, Serikali imeamua kudhibiti uingizaji, usambazaji na uuzaji wa rejareja wa tindikali zinazotumika viwandani, katika maabara na vyombo vya usafiri.

Kwa kuanzia, wameanza kutoa leseni maalumu kwa watumiaji halali kwa kuwasajili katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali huku wakipeleka mrejesho wa mauzo katika ofisi hiyo kila mwezi.

Hayo yalisemwa jana na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manywele alipozungumza na waandishi wa habari akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi.

Alisema kwa kuanzia, vibali vya kuagiza kemikali hizo lazima kuombwa upya ili kusimamia na kudhibiti huku takwimu za mauzo na jina la mnunuzi, tarehe aliyonunua, kiasi na ukali wa tindikali vikioneshwa.

Alisema taarifa hizo zitakuwa zikitumwa kwa Mkemia Mkuu kila mwezi kuanzia mwezi huu huku wauzaji wa rejareja wakipewa miezi mitatu kujisajili kwenye ofisi hizo.

"Pia wauzaji wanatakiwa kuwa na kumbukumbu za mauzo na alizonunua, namba ya leseni, kiasi na tarehe huku watumiaji katika vyombo vya usafiri wakitakiwa watoe malipo ya huduma kwani hawatatakiwa kununua na kuondoka na tindikali," alisema Manywele.

Aliongeza kuwa huduma hizo zitatolewa kwa wauzaji wa rejareja waliosajiliwa ambapo tindikali zitakuwa katika ujazo wa lita tano na kuendelea na kuanzia sasa hairuhusiwi kuuzwa chini ya ujazo huo.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo