Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Aisha Omari (kushoto) Mama wa watoto wawili waanga wa
mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8)
waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo
alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1,
2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa
Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. Katikati ni Balozi wa
Tanzania, nchini Kenya, Batrida Buriani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Aisha Omari, Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa
Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa
katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika
kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1,
2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa
Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao.PICHA NA OMR.