Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (wa pili
kulia|) akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Pwani leo Ijumaa (Agosti 2.
2013) wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Halima Kiemba
(kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Bertha Swai (wa pili kushoto).
Wajumbe wa Tume walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya
kupokea taarifa za maandalizi ya Mikutano ya Mabaraza ya Katiba katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani humo, kulia ni Mjumbe wa Tume,
Mhe. Al-shaymaa Kwegyir.
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi
akuizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya
Kibaha Mkoa wa Pwani wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo
(Ijumaa Agosti 2, 2013) katika uykumbi wa Shule ya Sekondari ya
Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani,
Bi. Fediria Swai akichangia hoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya
iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katika katika mkutano uliofanyika
leo( Ijumaa Agosti 3, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
Mjumbe
wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, Jenifer
Hassani akichangia hoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika leo Ijumaa (Agosti
2, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo
Wilayani humo.
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza
na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani
Pwa ni katika mkutano uliofanyika leo Ijumaa (Agosti 3, 2013) katika
ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
Wajumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto),
Al- Shaymaa Kwegyir (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
wa Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Halima
Kiemba (wa pili kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bi. Bertha Swai
mara baada ya Wajumbe wa Tume kupokea taarifa ya Maandalizi ya Mikutano
ya Mabaraza ya Katiba katika Halmashauri za Wilaya na Miji ya
Kibaha.(PICHA NA TUME YA KATIBA).