KUFUATIA WIZI WA MAMILIONI KARIAKOO, POLISI WATANGAZA DAU LA MILIONI 100

Kufuatia tukio la wizi lililotokea leo katika benki ya Habib African iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuibiwa zaidi ya shilingi milioni 900 za Tanzania, Jeshi la Polisi limetangaza dau la shilingi milioni moja kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi yaliyofanya hicho kitendo. 

Majambazi hayo yaliyokuwa yamevaa sare za Jeshi la Polisi yalivamia benki hiyo na kupora Dola za Kimarekani 181,885 sawa na shilingi milioni 293.9 za Tanzania. 

Pia yalipora jumla ya shilingi milioni 700 za Tanzania na kufanya jumla ya fedha zilizoibiwa kuwa shilingi milioni 993.9


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo