Katibu Mkuu mpya wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwasili
mbele ya jengo la PPF huku akipokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa Wizara
hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu mpya wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akipewa shada
la maua na Afisa Habari Mkuu Idara ya Habari, Bi. Mwanakombo Jumaa kama pongezi
kwa kupewa cheo cha Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
Laizer akilakiwa kwa shangwe na Mkurugenzi rasilimali watu Bw. Titus Mkapa
wakati wa hafla ya kupokelewa na kukabidhiwa kiti cha Unaibu Katibu Mkuu leo
jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
Laizer akipewa mashada ya maua baada ya kupokelewa na wafanayakazi wa Wizara ya
Habari kama pongezi ya kupewa cheo cha Unaibu.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
Laizer akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
aliyesimama katikati Bw.Clement Mshana, kulia kwake ni Kaimu Mhariri Mtendaji
Mkuu wa TSN Bw. Gabriel Ndelumaki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Assah Mwambene.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
Laizer akisalimiana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo wakati alipolakiwa
na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozana kwa
pamoja kuelekea ofisini.
Picha ya pamoja ya
Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda akitoa hotuba
fupi ya kukabidhi cheo kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani).Picha zote na Benedict Liwenga