Bwana shamba wa kampuni ya highlands seed growers Iddi Kapteni akiwagawia wakulima wa Makete mbegu bora kwa ajili ya kilimo mara baada ya kuwapa elimu ya namna ya kutumia mbegu hiyo ili wapate mavuno bora.
Mbegu bora na ya kisasa ya mahindi inayohimili hali ya
hewa ya mikoa yote ya nyanda za juu kusini inayozalishwa na kampuni ya
highland seed growers ya jijini Mbeya ambapo wakulima wa makete
wamepewa bure kwa ajili ya majaribio.
Mtangazaji wa Kitulo FM iliyopo Makete Conradi Mpila akipokea mbegu
Bwana shamba Iddi Kapteni akitoa maelekezo kwa wakulima wa Makete namna ya kutumia mbegu hiyo ili iwapatie mazao mazuri
Iddi Kapteni akionesha vipimo katika shamba darasa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwafundisha wakulima wa Makete
Msambazaji wa mbegu hizo Bw. Award Mpandila akitoa nasaha zake kwa wakulima wa Makete waliohudhuria shamba darasa
Msambazaji wa mbegu Tito Tweve ambaye ni wakala aliyeidhinishwa na kampuni ya Highland na halmashauri ya wilaya ya Makete akionesha viashiria vya kutambua mbegu halisi na feki
Mkulima Jeita Mahenge kutoka kijiji cha Isapulano Makete akifurahia baada ya kupewa mbegu bure
Kaimu afisa kilimo mifugo na ushirika wilaya ya Makete Beda Kusenge akizungumza namna walivyojipanga kuzuia uingizaji wa mbegu feki za kilimo wilayani mwake
Mwakilishi wa afisa pembejeo wilaya ya Makete Lazaro Moses akiwahakikishia wakulima hao kuwa pembejeo za kilimo kwa mwaka huu tayari zimefika Makete kwa wakati
Wakulima wakifurahia mbegu walizopewa bure